Katekisimu ni muhutasari wa mafundisho yote ya Kanisa Katoliki mintarafu imani na maadili. Kusema hivyo kwa maneno ya Papa Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili: “Tunaposoma Katekisimu ya Kanisa Katoliki, tunaweza kuutambua Umoja wa Ajabu wa Fumbo la Mungu.”
Jimbo Kuu Katoliki Arusha linatoa Elimu ya Dini kwanza kwa Shule za Msingi na Sekondari pamoja na Vyuo. Pili, inahakikisha ukateketisi sahihi unaanzishwa na kupangwa katika Parokia na katika Vituo vya Misheni.
Jimbo Kuu Katoliki Arusha pia hutoa mafunzo endelevu kwa makatekista (walimu wa dini), kuwaunga mkono katika mafundisho yao na tathmini ya kazi zao. Kwa kuongeza, semina za kufundisha na kozi za kujiendeleza hutolewa. Idara inayohusika inaongozwa na Sr. Joyce Maria (CDNK) akisaidiwa na Katekista Frank Mollel.
Sr. Joyce Maria pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Katekesi.