Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU KWA AJILI YA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KANISA JIPYA LA PAROKIA YA FAMILIA TAKATIFU, NJIRO

ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU KWA AJILI YA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA KANISA JIPYA LA PAROKIA YA FAMILIA TAKATIFU, NJIRO

Katika siku yenye baraka ya tarehe 12 Januari 2025, wakristo wa Parokia ya Familia Takatifu, Njiro, walikusanyika kwa shangwe na furaha kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la kanisa jipya. Tukio hili adhimu liliendana na kumbukumbu ya Ubatizo wa Bwana wetu Yesu Kristo, likiwa sehemu ya maadhimisho ya Jubilei Takatifu ya mwaka 2025 yenye kauli mbiu “Mahujaji katika Matumaini”

Misa hiyo iliongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac Amani, ambaye katika homilia yake aliwasihi waamini kutambua thamani ya kanisa kama sehemu ya kujichotea neema na kukua kiroho. Alisisitiza kuwa kila mmoja anapaswa kumrudia Mungu kwa moyo wa unyenyekevu na kuishi maisha ya utakatifu, akitolea mfano wa Yesu Kristo aliyekaa mafichoni hadi alipoanza utume wake akiwa na umri wa miaka 30, kama tunavyoelezwa katika Injili ya Luka Mtakatifu.

Mhashamu Askofu Mkuu aliwakumbusha waamini kuwa ujumbe wa Injili, kama ulivyoandikwa na Marko, unatoa mwaliko wa kutubu na kuamini Injili, hatua inayotufanya kuwa warithi wa Ufalme wa Mungu. “Ubatizo ni hatua ya kuzaliwa mara ya pili kwa njia ya Roho Mtakatifu,” alieleza, akiongeza kuwa, “Dhambi na utakatifu ni vitu viwili tofauti visivyoweza kuchangamana. Pale unapogundua umekosea mbele za Mungu, nenda ukatubu.”

Wito wa Utakatifu na Umoja

Mhashamu Askofu Mkuu Isaac Amani alitoa wito wa kuishi maisha yanayoakisi mafundisho ya Yesu Kristo kwa kusameheana kwa dhati, kupendana kwa roho na kweli, na kuonyesha huruma kwa wote. Aliwaasa wazazi kuwafundisha watoto wao kukabiliana na changamoto za maisha kwa kuwa maisha hubadilika na anayejua kesho ni Mungu pekee.

Jubilei 2025: Mwito wa Kuimarisha Imani

Katika maadhimisho hayo, waamini walihimizwa kutumia Jubilei ya mwaka 2025 kama fursa ya kuimarisha imani, kuwa mahujaji wa kweli na kuishi kikamilifu katika wito wa ubatizo wao. “Tukumbuke wema wa Mungu na tuendelee kumtegemea Yeye kama msingi wa maisha yetu,” alihitimisha.

Tukio hili la kihistoria linaacha alama kubwa kwa waamini wa Parokia ya Familia Takatifu, Njiro, likiwa ni ishara ya matumaini mapya na mwendelezo wa imani katika safari ya kiroho. Wote walihimizwa kushiriki kwa moyo wote katika ujenzi wa kanisa hili jipya, ambalo litakuwa chemchemi ya neema na makazi ya kiroho kwa vizazi vijavyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*