Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

MISA TAKATIFU KWAAJILI YA KUZIOMBEA FAMILIA TAKATIFU

SHIRIKA LA UTOTO MTAKATIFU JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA WAADHIMISHA MISA TAKATIFU KWAAJILI YA KUZIOMBEA FAMILIA TAKATIFU

Shirika la Utoto Mtakatifu Jimbo Kuu Katoliki Arusha limefanya tukio la kipekee la kuadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kuziombea familia takatifu. Ibada hii imefanyika katika Dekania ya Jiji Mashariki, Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mtume, Baraa-Moshono. Tukio hilo lilianza kwa watoto wa Shirika hilo kusali Rozari kabla ya Misa hiyo maalum.

Adhimisho hilo limekuja kama sehemu ya ufumbuzi wa Novena ya Rozari ya Siku Tisa, ambayo ilianza tarehe 11 Oktoba 2024 na itahitimishwa tarehe 20 Oktoba 2024. Misa hiyo imeongozwa na Padre Lion Auxence SMA, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mtume, Baraa-Moshono. Padre Lion aliwaomba walezi kuendelea kuwafundisha watoto namna ya kusali Rozari, hasa kwa ajili ya familia zao, na akawahimiza watoto hao kuwafundisha wenzao ambao bado hawajapata mafundisho hayo.

Akizungumza wakati wa Misa hiyo, Padre Lion alisema, “Watoto wa Kipapa waendelee kusali Rozari kila siku, ili waimarike kiroho na pia kuwafundisha watoto wenzao. Bikira Maria atasikia sala zenu, kwani Yesu Kristo alisema waacheni watoto wadogo waje Kwangu, maana Ufalme wa Mbinguni ni wao.”

Zaidi ya watoto 3,000 wa Kipapa kutoka Jimbo Kuu Katoliki Arusha walihudhuria adhimisho hili, likiwa ni sehemu ya maandalizi ya tukio kubwa la kuadhimisha miaka 50 ya Upadre wa Baba Askofu Mkuu, Isack Amani wa Jimbo Kuu Arusha. Tukio hilo la kihistoria litafanyika tarehe 26 Novemba 2024 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Fransisko wa Asizi, Ngulelo.

Waumini, wazazi, na walezi wamehimizwa kuendelea kuwalea watoto katika maadili mema, ili waweze kukua katika imani na kuepukana na changamoto za utandawazi zinazoathiri vijana wengi katika nyakati za sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*