Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

UMOJA WA MADHEHEBU WAUNGANA ARUSHA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA NA ISRAEL

 UMOJA WA MADHEHEBU WAUNGANA ARUSHA KULIOMBEA TAIFA LA TANZANIA NA ISRAEL

Katika juhudi za kuliombea taifa la Tanzania pamoja na Israel, viongozi wa madhehebu mbalimbali walikusanyika kwa maombi maalum yaliyofanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT). Kongamano hilo lililoanza tarehe 14 hadi 19 Oktoba 2024, liliwaleta pamoja viongozi mbalimbali wa dini nchini Tanzania, wakiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha na Mwenyekiti Msaidizi wa Umoja wa Madhehebu ya Kikristo Tanzania, Mha. Isaac Amani.

Katika hotuba yake, baba Askofu Isaac Amani alisisitiza umuhimu wa kanisa kuombea taifa na kuimarisha umoja ndani ya jamii za Kikristo. “Sisi kama kanisa la Arusha, tunapaswa kuliombea taifa letu. Wakristo tunapaswa kuwa na umoja, kwani umoja ni uti wa mgongo wa kanisa. Bila umoja, huduma yetu haina tija” alieleza.

Akitoa rejea ya maandiko kutoka Injili ya Yohana 17:21, alisema, “Yesu Kristo aliomba ili wote wawe na umoja kama Baba alivyo ndani yake, nasi pia tuwe ndani yao, ili ulimwengu uamini kuwa Yeye ndiye aliyetumwa. Umoja huu ndiyo msingi wa mafanikio yetu kama kanisa.”

Aidha, Mha. Isaac Amani alisisitiza umuhimu wa maisha ya Kikristo ndani ya familia, jamii, na siasa, akiwahimiza waumini kuwa na mioyo ya upendo na kushikamana na wenzao wa madhehebu mengine kama ndugu. Alikumbusha pia umuhimu wa kuongozwa na Roho Mtakatifu, tuliyepokea katika ubatizo, ili kutenda mema na kuishi kwa mshikamano.

Akihitimisha, aliwataka waumini kukumbuka jinsi kanisa lilivyozaliwa siku ya Pentekoste (Matendo ya Mitume 2:1-13) na kusimama kwa pamoja katika maombi, kwa kuzingatia kuwa “waliposimama wawili au watatu, Mungu yuko katikati yao.”

Kwa msingi huo, alitoa wito kwa Wakristo wote kuendelea kuombeana na kusimama imara katika imani moja kwa ajili ya taifa na ulimwengu kwa ujuml

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*