Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

UMOJA WA VYAMA VYA KITUME NA MASHIRIKA YA JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA WAFUNGUA MWAKA 2025 KWA ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU

UMOJA WA VYAMA VYA KITUME NA MASHIRIKA YA JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA WAFUNGUA MWAKA 2025 KWA ADHIMISHO LA MISA TAKATIFU

Tarehe 11 Januari 2025, Umoja wa Vyama vya Kitume na Mashirika mbalimbali ya Jimbo Kuu Katoliki Arusha wameadhimisha Misa Takatifu ya kufungua rasmi mwaka mpya katika Parokia ya Mtakatifu Ambrose Kibuka – Sinon. Adhimisho hili limeongozwa na Dekano wa Dekania ya Arumeru, Padri Rafael Msimbi, ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Nambala, akishirikiana na mlezi wa Vyama vya Kitume Jimboni, Padri Willbard Mayunga, pamoja na mapadre wengine kutoka ndani na nje ya parokia.

Katika mahubiri yake, Padri Rafael Msimbi amesisitiza umuhimu wa waamini wa Vyama vya Kitume kuishi kikamilifu utume wao kama mahujaji wa kweli, hasa katika mwaka huu wa Yubilei wa Mwaka Mtakatifu 2025. “Tuendelee kuwa mashahidi wa kweli wa imani yetu kwa kueneza Neno la Mungu, kuishi kwa maombi na kuwa watu wa upendo kwa kila mmoja” alihimiza.

Padri Msimbi pia alitoa wito kwa waimbaji wa kwaya, wanakarismatiki na wanachama wa vikundi mbalimbali vya kitume kama WAWATA, UWT, Utoto Mtakatifu na wengine, kufanya kazi zao kwa moyo safi na utiifu. “Kila mmoja wetu amepewa zawadi ya kipekee na nafasi ya kumtumikia Mungu; tumieni vipawa vyenu kwa roho na kweli ili kufanikisha kazi ya Uinjilishaji” alisema.

Baada ya Misa, Padri Willbard Mayunga, mlezi wa Vyama vya Kitume Jimboni, aliwapongeza wanavyama wote kwa kujitokeza kwa wingi na kwa kuonyesha mshikamano wa imani. Pia aliwasihi waendelee kujitoa kwa kazi ya utume kwa maneno na matendo yenye uwajibikaji. “Maneno na matendo lazima yaendane; bila hivyo, kazi zetu zinakuwa bure. Tuishi kwa kupendana na kushirikiana, kwani mtu bila watu ni kazi bure” aliongeza.

Adhimisho hili limeleta mshikamano mkubwa miongoni mwa waamini wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, huku likiwa ni mwanzo wa safari ya kiroho katika mwaka wa Yubilei Mtakatifu wa 2025. Kila mshiriki amepewa changamoto ya kuendeleza mshikamano, maombi na huduma kwa jamii katika safari ya kumtumikia Mungu.

Tukitegemea Mungu kwa kila jambo, tutafaulu” alihitimisha Padri Msimbi, akiwahamasisha waumini wote kuendelea kuwa mashahidi wa kweli wa upendo na utume wa Kanisa Katoliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*