Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

(WAWATA) JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA WAADHIMISHA MISA YA SOMO WAO

WAWATA JIMBO KUU KATOLIKI ARUSHA WAADHIMISHA MISA YA SOMO WAO

WAWATA (Wanawake Wakatoliki Tanzania) Jimbo Kuu Katoliki Arusha wameadhimisha Misa Takatifu ya somo wao, Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni, tarehe 29 Septemba 2024 katika Parokia ya Mtakatifu Luca, Enduleni, Wilaya ya Ngorongoro, Mkoani Arusha.

Misa hiyo iliongozwa na Mhashamu Baba Askofu Mkuu Isaac Amani, ambapo katika mahubiri yake alisisitiza umuhimu wa waumini kuwa makini katika kutafuta na kutumia mali kwa uangalifu, kwa mfano wa WAWATA ambao wamekuwa chachu ya maendeleo ya kiimani na kijamii kwenye jumuiya mbalimbali.

Askofu Amani aliwasihi waumini wote kuiga mfano wa WAWATA katika kuleta maendeleo kwa umoja na ushirikiano, huku wakihamasisha watu kusali pamoja katika jumuiya na kusaidiana kama familia ya Kanisa. Alisema, “Waumini wote tuige mfano wa WAWATA kwa namna wanavyopambana kwa umoja kuleta maendeleo na kusaidiana katika jamii, hasa wao kama akina mama.”

Aidha, Askofu Amani aliwataka WAWATA kuwaombea wanachama wa UWAKA (Umoja wa Wanaume Wakatoliki) ili nao waweze kufikia kiwango cha uinjilishaji na kupeleka Neno la Mungu kwa watu katika jamii na familia. Alisisitiza kuwa, “Waombeeni pia UWAKA wapate mwamko wa kuinjilisha, maana wao ni vichwa vya familia.”

Pia, aliwahimiza waumini kusimama imara kuliombea Kanisa na kuwaombea wale wasiokuwa Wakristo lakini wanajitahidi kutenda matendo mema kusaidia jamii. Aliongeza kuwa, “Simameni katika kuliombea Kanisa na kuwaombea waumini wengine ambao si Wakristo lakini wanatenda mema ili nao wasipotee katika dunia ya sasa.”

Katika hitimisho lake, Askofu Amani aliwataka waumini kumtazama mtoto wa kike na kumsimamia lakini pia kutomwacha mtoto wa kiume, akisema kuwa watoto wa kiume wanapoachwa wanakumbwa na changamoto nyingi na kujiingiza katika matendo maovu. Alihimiza jamii kuwalea watoto wote kwa maadili mema na kuheshimiana ili kujenga jamii bora.

Alisisitiza kuwa ni muhimu jamii kusimama imara kulinda maadili na tamaduni, huku wakiomba msaada wa Mungu ili waendelee kuishi kwa amani na mshikamano nchini Tanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*