Fortunatus M. Lukanima ( 8 Desemba 1940 – 12 Machi 2014 ) alikuwa Askofu wa pili wa Kanisa Katoliki Jimbo la Arusha . Baada ya Askofu Durning kustaafu kama Mchungaji wa familia ya Mungu Jimbo Katoliki la Arusha Agosti 26, 1989; Jimbo hilo iliasisiwa na Askofu wa Tanzania Mhashamu Askofu Fortunatus M. Lukanima ambaye alipewa daraja ya Upadre mwaka 1968 na kuteuliwa mwaka 1989 kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Arusha. Alijiuzulu mnamo 1998.