Maono Yetu
- Familia ya Mungu inayoishi kulingana na Injili ya Kristo.
Utume Wetu
- Kujenga familia ya Mungu inayoishi katika Upendo, Uwajibikaji na Mshikamano kwa njia ya kueneza Injili na kutoa huduma za Kiroho na Kijamii kwa mujibu wa mafundisho ya Kikatoliki.
Maadili yetu ya Msingi
- Upendo, Umoja, Huduma, Haki na Amani, Heshima na ulinzi kwa maisha na uadilifu wa maisha, Uwazi na Uwajibikaji, Maisha ya sala.
![](https://arusha-archdiocese.or.tz/wp-content/uploads/2023/11/RAMANI-scaled-e1699435575463-768x959.jpg)
Kuhusu sisi
Jimbo Katoliki la Arusha
Jimbo Katoliki Arusha lilianzishwa Machi 1, 1963, na kusajiliwa rasmi kuwa Bodi ya Wadhamini ya Jimbo Katoliki Arusha Juni 17, 1965. Tarehe 16 Machi, 1999, Jimbo la Arusha lilipandishwa hadhi kuwa Jimbo Kuu Katoliki Arusha na Wizara ya Mambo ya Ndani. Tarehe 22 Julai 2002 Jimbo lilisajiliwa tena na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa namba SO Na. 8848
Ofisi Kuu ya Jimbo iko katika eneo la Parokia ya Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu ambapo Kanisa Kuu liko katika hatua ya kukamilika.
MAASKOFU