Askofu Mkuu Mstaafu Josaphat Louis LEBULU. Alizaliwa tarehe 13 Juni 1942 katika Parokia ya Kisangara Juu Jimbo la Same, moja ya majimbo dada ya Jimbo Kuu Arusha. Alipadrishwa tarehe 11 Desemba 1968 na kumweka wakfu Askofu wa Same tarehe 24 Mei 1979. Aliteuliwa Msimamizi wa Kitume wa Jimbo la Arusha tarehe 20 Agosti 1997 na Desemba 9, 1998 aliteuliwa Askofu wa Arusha na kusimikwa rasmi tarehe 31 Januari 1999. 24 Machi 2000 aliteuliwa Askofu Mkuu wa Kwanza wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha. Watangulizi wake Hayati Askofu Mstaafu Fortunatus M. Lukunima (1988-1997) na Askofu Dennis Vincent Durning wa Shirika la Roho Mtakatifu askofu wa kwanza tangu 1963 hadi 1988.