Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

Mha. Prosper B. Lyimo

Mha. Prosper B. Lyimo

Askofu Msaidizi Jimbo Kuu Katoliki Arusha

Mhashamu Baba Askofu Prosper Baltazar Lyimo ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Arusha. Alizaliwa Kyou Kilema -Moshi mwaka 1964. Baada ya masomo yake ya Shule ya Msingi katika Shule za Msingi za Maua na Ngurdoto mkoani Kilimanjaro na Arusha, alijiunga na masomo ya Sekondari katika Seminari Ndogo ya Jimbo Kuu – Mtakatifu Thomaso wa Akwino huko Oldonyo Sambu Arusha. Alifanya Masomo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mama wa Malaika, Kibosho-Moshi, na Taalimungu katika Seminari ya Kijimbo ya Mtakatifu Paulo – Kipalapala mkoani Tabora. Alipadrishwa tarehe 4 Julai 1997. Baada ya upadrisho aliteuliwa mlezi katika Seminari Ndogo ya Mtakatifu Thomaso wa Akwino na baadaye Katibu Mkuu wa Jimbo na wakati huo huo mtumishi katika Mahakama ya kanisa. Mwaka 2004 alikwenda Roma kwa masomo zaidi ya Sheria ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Urbanian na kumaliza masomo ya uzamili katika Sheria za Kanisa mwaka 2007. Mwaka 2008 alikwenda Kanada kwa masomo zaidi juu ya Sheria ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Mt. Paul na kumaliza masomo katika kiwango cha Uzamivu (PhD) Juni 2 2012. Aliteuliwa na papa Benedikti XVI kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha mwaka 2014 na aliwekwa wakfu tarehe 15 Februari 2015.