Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

WAKRISTO WAKUMBUSHWA KUMSHUKURU MUNGU – PADRE SIYO KAZI BALI NI WITO WA KIUNGU

Julai 12, 2025

Katika hali ya shukrani, tafakari, na mshikamano wa kiroho, waamini wa Kanisa Katoliki walikusanyika katika Kanisa la Moyo Safi wa Bikira Maria – Ungalimited, Jimbo Kuu Katoliki Arusha, kwa ajili ya Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mapadre wapya wawili, Padre Henry Kyara na Padre Frank Monorua. Hawa ni kati ya Mapadre 16 waliowekwa wakfu tarehe 10 Julai 2025 na Mhadhamu Isaac Amani, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu.

Katika mahubiri ya Misa hiyo, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, alitumia nafasi hiyo kutoa wito mzito kwa waamini wote: “Tujifunze kuwa na moyo wa shukrani kwa Mungu katika maisha yetu ya kila siku.”

Askofu Mchamungu alisema kuwa moyo wa shukrani ni ishara ya utambuzi wa neema za Mungu, na akasisitiza kuwa mtu asiye na shukrani hukosa baraka.

“Tufurahie, tusali bila kuchoka. Tukumbuke mfano wa wakoma 10 walioponywa na Yesu ni mmoja tu aliyerudi kushukuru. Nasi tujifunze kuwa kama yule mmoja,” alisema Askofu.

Wito wa Upadri ni Zawadi ya Mungu, Siyo Cheo cha Dunia

Askofu Mchamungu alieleza kuwa wito wa Upadri si ajira ya kawaida, bali ni mwito wa kipekee kutoka kwa Mungu mwenyewe.

“Si kila mtu anaweza kuwa padre. Ni Mungu peke yake ndiye anayechagua. Kazi hii ni ngumu na ya kujitoa mhanga,” alisisitiza.

Aliwataka mapadre wote, wapya na wale walioko kazini, kusimama imara katika sala na tafakari ya kina ya maisha ya Kristo, kwani bila hayo, ni vigumu kuendelea na kazi ya utume wa kipadre.

Mapadri Waaswa Kumtii Askofu na Kuwatumikia Waamini

Katika kuendeleza mafundisho ya Kanisa, Askofu Mchamungu aliwakumbusha mapadri kwamba wanapaswa kufanya kazi chini ya mamlaka ya Askofu wao, wakitekeleza wajibu wao wa kichungaji kwa unyenyekevu na utii.

“Padri ni mtumishi wa Mungu anayewatumikia waamini. Mamlaka aliyonayo yametolewa na Kristo kupitia kwa Askofu wake. Tii ni msingi wa utume,” alieleza.

Wazazi Watambue Miito ya Watoto Wao

Akizungumzia nafasi ya familia katika kusaidia miito ya kipadri na kitawa, Askofu aliwahimiza wazazi kuwa makini katika kutambua dalili za wito kwa watoto wao.

“Ukiona mwanao anaanza kuvaa kiremba, ujue kuna sister anachipua. Na anapoanza kusema maneno ya Kipadre, fahamu yuko njiani kuwa kuhani. Msaidie kwa maombi na malezi ya kiroho,” alisema kwa msisitizo.

Mama Bikira Maria Aendelee Kuwa Mlinzi wa Mapadri

Askofu Mchamungu alihitimisha mahubiri yake kwa kuwaalika waamini wote kuwaombea Mapadri wapya na wote walioko katika wito huu mtakatifu. Aliwakabidhi kwa Mama Bikira Maria, mama wa Yesu na Kanisa, ili awasimamie na kuwaombea daima.

“Kazi ya Upadri ni ngumu na ina upinzani mkubwa. Bila maombi, hawataweza kusonga mbele. Tuwaombee waendelee kuwa waaminifu na watumishi wa kweli wa Injili,” alisema kwa unyenyekevu mkubwa.

Tukio hili la Misa ya Shukrani lilikuwa zaidi ya adhimisho la liturujia  lilikuwa ni darasa la imani, sala na tafakari kwa kila Mkristo. Ni kumbusho kuwa zawadi ya wito ni ya thamani kubwa, na ni wajibu wetu wote kuishukuru, kuiheshimu na kuikuza kwa sala, mshikamano na ushirikiano.

Mungu aendelee kuwaita, kuwaweka wakfu, na kuwaimarisha watumishi wake katika shamba lake. Tumsifu Yesu Kristo!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*