Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

MTAKATIFU ANNA WAADHIMISHA MISA TAKATIFU YA SOMO WA PILI WA SHIRIKA LA MTAKATIFU MONIKA

MTAKATIFU ANNA WAADHIMISHA MISA TAKATIFU YA SOMO WA PILI WA SHIRIKA LA MTAKATIFU MONICA 08/09/2024

Mtakatifu Anna ameadhimisha Misa Takatifu ya somo wa pili wa Mtakatifu Monica katika sherehe iliyoambatana na maadhimisho hayo, ambapo somo wa kwanza alikuwa Mtakatifu Anna mwenyewe. Sherehe hiyo imefanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu, Jimbo Kuu Katoliki Arusha, na kuongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Mhashamu Isaac Amani.

Katika mahubiri yake, Askofu Amani alisisitiza umuhimu wa Wakristo kuishi kwa kujali utu wa binadamu, akieleza kuwa Mungu anapenda tuishi katika uhuru wa kweli. Alisema kuwa, wale wanaomwamini Mungu wanapaswa kuheshimu utu wa wengine na kutowadharau, huku wakijikita katika upendo na kujitenga na utumwa wa vitu vya kidunia.

“Wakristo tukumbuke Mungu anatupenda, na anataka tuishi kwa kujali utu wa wengine. Tupende, tusifarakane, na tuwe na matumaini kwa Mungu. Hakikisha umejiandaa vyema ili kupata urithi wa milele ukiwa msafi kiroho,” alisema Askofu Amani.

Aliendelea kusisitiza kuwa jamii inategemeana, na hivyo tajiri asiwaache maskini, wala maskini wasimdharau tajiri. Aliwataka waumini kuwekeza katika mambo ya Kristo, wakisherehekea uhuru wao na kuruhusu wengine kufurahia uhuru huo pia.

“Furahia uhuru wako, na umpe mwenzako uhuru. Uwe tayari kumsaidia mwenzako kama walivyofanya Mtakatifu Anna na Mtakatifu Monica, ambao walimwombea kwa upendo mme wa Monica na mwanawe, Mtakatifu Agustino,” aliongeza.

Askofu Amani aliwataka Wakristo kuiga mfano wa Mtakatifu Monica na Mtakatifu Anna, kwa kuwaombea familia zao. Alikumbusha jinsi Mtakatifu Monica alivyomwombea mwanawe, Askofu Agustino, hadi akaongoka, kuwa askofu na hatimaye Mtakatifu. Aliwasihi Wakristo kusimama imara katika kumtetea Kristo aliyefilia msalabani kwa ajili ya wote.

Sherehe hiyo ya kiroho ilihudhuriwa na waumini wengi waliokuja kuadhimisha maisha na imani ya watakatifu hawa wawili wakubwa katika historia ya Kanisa Katoliki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*