Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

WAZEE WASTAAFU WA SHIRIKA LA MT. AGUSTINO WAADHIMISHA MISA TAKATIFU KUMUENZI MTAKATIFU AGUSTINO

WAZEE WASTAAFU WA SHIRIKA LA MT. AGUSTINO WAADHIMISHA MISA TAKATIFU KUMUENZI MTAKATIFU AGUSTINO 01/09/2024

Wazee wastaafu wa Shirika la Mtakatifu Agustino kutoka Jimbo Kuu Katoliki Arusha wameadhimisha Misa Takatifu kwa ajili ya kumuenzi Mtakatifu Agustino, somo wao wa shirika hilo, katika Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Ungalimited. Adhimisho hilo liliongozwa na Katibu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Padri Wensenslaus Wenga, ambaye aliwahimiza waumini kuishi kwa uaminifu katika dini yao ya Kikristo na kuacha mchanganyo, akisisitiza kuwa Yesu Kristo hapendi hali hiyo.

“Katika Misa hii Takatifu, tuwe na imani moja na tumwamini Yesu Kristo. Tukoleze imani yetu ya Katoliki na tuilinde. Ninyi wazee ndiyo hazina ya kesho, mnatakiwa kuwashauri wale ambao imani zao bado ni changa, na muwe na moyo wa kusaidia wasiojiweza, kwani hayo ndiyo mambo Mungu anayoyapenda siku zote,” alisema Padri Wenga.

Padri Wenga aliendelea kwa kuwaasa Wakristo kujifunza kuweka maagano yao upya na Bwana Yesu Kristo ili wawe wafuasi wake wa kweli siku atakaporudi kukomboa ulimwengu. Aliwataka Wakristo waishi kwa utakatifu, wakijitakasa kiroho, huku wakijitahidi kufuata sheria za Mungu na kuthamini wokovu wao.

“Shikeni sheria za Bwana wetu Yesu Kristo na tujifunze kuweka maagano yetu naye ili tuwe wafuasi wake wa kweli. Tukumbuke jinsi alivyoutoa uhai wake kwa ajili ya dhambi zetu,” alisisitiza.

Misa hiyo pia ilihudhuriwa na Padri Willbard Mayunga, Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Kichungaji, ambaye alimwakilisha Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Mhashamu Isack Amani. Padri Mayunga aliwapongeza wanashirika wa Mtakatifu Agustino kwa kujitokeza kwa wingi na kuendelea kutumikia shirika hilo hata katika uzee wao.

“Nawashukuru wanashirika wote wa Mtakatifu Agustino kwa kujitokeza katika adhimisho hili la Misa Takatifu. Mungu azidi kuwabariki katika uzee wenu, na kwa yale mliyoyasikia katika homilia ya Katibu Mkuu, myatunze na kuyaishi kama wazee wastaafu,” alisema Padri Mayunga.

Kwa upande wake, Paroko wa Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria, Padri Festus Mangwangi, alimshukuru Askofu Isaac Amani kwa kuwatuma wawakilishi wake, akisema kuwa waliowakilisha ni kama Askofu mwenyewe na kwamba ni neema kubwa kwa parokia hiyo kupokea wageni hao kwa ajili ya adhimisho hilo.

“Asante Baba Askofu kwa kuwatuma wawakilishi wako na wazee wa Shirika la Mtakatifu Agustino. Ugeni huu ni baraka kubwa kwa Parokia yetu ya Moyo Safi na tumewapokea kwa mikono miwili,” alisema Padri Mangwangi.

Wazee wastaafu wa shirika hilo waliwashauri vijana wa Kanisa kuishi kwa utakatifu, wakiepuka vishawishi vya utandawazi ambavyo vimewapoteza wengi. Pia waliwaalika wanachama wapya, haswa wale waliofikisha umri wa miaka 50, kujiunga na shirika hilo ili kuwafundisha vijana maadili na kuwaongoza kwenye njia ya wokovu.

“Tunawakaribisha wanachama wapya kujiunga na Shirika la Mtakatifu Agustino. Kama umefikia miaka 50, jiunge nasi ili kuwafundisha vijana maadili ili nao wafikie umri wa uzee bila kuharibika, kwani dunia hii bila kuwa karibu na Yesu Kristo ni bure,” alisema mmoja wa mwanashirika.

Wazee wastaafu walimalizia kwa kusema kuwa imani yao kama Wakristo lazima ilindwe kwa maombi, kwani bila msaada wa Mungu, haiwezekani. Walihimiza waumini kuiga mfano wa Mtakatifu Agustino, ambaye alitambua makosa yake, akaongoka, na kuishi maisha yake yote kwa kumtumikia Yesu Kristo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*