Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

ASKOFU ISAAC AMANI: NUSU KARNE YA HUDUMA TAKATIFU

Julai 20, 2025

Katika tukio la kihistoria na la kipekee, waumini wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha na wageni kutoka maeneo mbalimbali walikusanyika kwa shangwe na mshikamano mkubwa kusherehekea Jubilei ya Miaka 50 ya Upadre wa Mhashamu Askofu Mkuu Isaac Amani Massawe. Misa Takatifu ya shukrani iliadhimishwa na Mhashamu Askofu Amani mwenyewe, ikiwa ni alama ya nusu karne ya utumishi wa kipekee katika shamba la Bwana.

Misa hiyo imehudhuriwa na Maaskofu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), mapadre kutoka ndani na nje ya jimbo, watawa wa kiume na wa kike, mashemasi, mafrateri pamoja na waumini wengi waliokusanyika kwa upendo na mshikamano.

Akitoa homilia katika adhimisho hilo, Mhashamu Askofu Rogath Kimario wa Jimbo Katoliki Same, alimwelezea Askofu Isaac Amani kama “chombo cha Mungu kama Ibrahim”, aliyekuwa tayari kuitikia wito wa Bwana kutoka katika maisha ya kawaida na kujitosa katika huduma ya kiroho kwa uaminifu na uvumilivu wa hali ya juu.

Askofu Kimario alikumbusha Injili ya Yohane 6, ambapo Yesu anasema: “Mimi ni chakula cha uzima. Atakayekula mwili wangu atakuwa na uzima wa milele.” Kwa kufuatilia maneno haya, alisisitiza kwamba Askofu Isaac Amani amekuwa chombo cha kugawa Ekaristi Takatifu kwa waamini kwa uaminifu mkubwa kwa kipindi cha miaka 50, akiendeleza kazi ya Kristo kwa sadaka, upole na hekima.

Askofu Kimario aliendelea kusisitiza kuwa Askofu Amani si tu kiongozi wa kiroho, bali pia ni daraja la amani, mshikamano na majadiliano ya kiekumene, akiunganisha madhehebu mbalimbali na kusaidia kujenga umoja wa Kikristo ndani na nje ya Jimbo Kuu Katoliki Arusha.

“Kaulimbiu yake ya ‘Kujitambua na Kushirikiana na Kristo kwa Matendo’ si kauli tu, bali ni mwanga ulioangaza maisha na utume wake. Tunaiona kiu yake ya kulitumikia Kanisa katika uhalisia wa matendo – katika mafundisho, huduma, na mshikamano wa kiimani,” aliongeza Askofu Kimario.

Akimhitimisha hotuba yake kwa heshima na taadhima, Askofu Kimario alisema:
“Kama Ibrahim baba wa imani alivyojitoa kwa Mungu kwa imani thabiti, vivyo hivyo Askofu Isaac Amani ni kielelezo hai cha mtu anayelishika agano la Bwana kwa moyo wa utumishi na wito safi. Yeye ni chombo cha Mungu katika kulitumikia Kanisa la ulimwengu.”

Kwa hakika, Askofu Mkuu Isaac Massawe Amani anabaki kuwa kiongozi wa kipekee, Askofu wa nne kuliongoza Jimbo la Arusha tangu kuanzishwa kwake mwaka 1963, na Askofu wa pili tangu Jimbo hilo lipandishwe hadhi kuwa Jimbo Kuu mwaka 1999. Maisha yake ya Upadre kwa kipindi cha miaka 50 ni ushuhuda wa upendo wa Mungu na wito wa kweli wa kikuhani.

Hongera Mhashamu Askofu Mkuu Isaac Amani. Umevuka nusu karne ya Utume kwa uaminifu.
Uwe mwanga kwa kizazi kijacho cha watumishi wa Kanisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*