Become A Donor

Become A Donor
Lorem Ipsum is simply dummy text of the printing and typesetting industry.

Contact Info

684 West College St. Sun City, United States America, 064781.

(+55) 654 - 545 - 1235

info@zegen.com

WAKRISTO WAHIMIZWA KUWA NA AMANI NA WATU WOTE

Isaac Amani

Katika Dominika ya 14 ya Mwaka C wa Kanisa, Mama Kanisa ametualika kwa namna ya kipekee kuishi katika amani na watu wote. Katika kuenzi mwaliko huo wa Kiinjili, Mhashamu Isaac Amani, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, amewaasa waamini kudumu katika sala na kuombeana ili waendelee kushikamana na mafundisho sahihi ya Kanisa Katoliki, akionya vikali dhidi ya kutangatanga kiimani,  jambo alilolieleza kuwa si sifa ya Mkristo anayejitambua.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Misa Takatifu ya Kipaimara katika Parokia ya Mtakatifu Fransisko wa Asizi Ngulelo, ambapo watoto 163 walipokea Sakramenti hiyo takatifu, Mhashamu Amani aliwataka waamini wote, hususan wazazi, kutimiza kwa dhati majukumu yao ya malezi ya kiroho na kimwili. Alisisitiza kuwa familia ni shule ya kwanza ya imani, hivyo wazazi hawapaswi kuwa na haraka ya kutafuta mali kiasi cha kusahau kuwalea watoto wao katika misingi ya imani ya Kanisa Katoliki.

Kila mzazi Mkristo anapaswa kumpa mtoto jina la Mtakatifu kulingana na siku aliyozaliwa ,jina lenye maana ya kiimani, si la mitindo au maarufu tu. Huo ndio utambulisho wa imani yetu” alisema Askofu Mkuu Isaac Amani.

Aidha, aliwakumbusha watoto waliopokea Kipaimara kuwa wanalo jukumu la kuyaishi mafundisho ya Kanisa, kuhubiri habari njema na kuwa kielelezo cha wema kwa wenzao. Aliwaonya dhidi ya kuwa kama “mbwa mwitu” wanaotumia maneno mengi pasipo tafakari, badala yake aliwataka kuwa “kondoo wa Kristo” wanaoongozwa na Roho Mtakatifu na kuyatumia mapaji saba waliyoyapokea kama dira ya maisha yao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Parokia hiyo, akizungumza kwa niaba ya wazazi na walezi, alisisitiza kuwa mafanikio ya malezi ya kiimani hutegemea sana msimamo na usimamizi wa wazazi. “Malezi yanaanza tangu utotoni. Mtoto wa leo ndiye mzazi wa kesho, na kama hatapata msingi mzuri sasa, hatakuwa na uwezo wa kumlea vyema mtoto wake baadaye” alionya.

Alihitimisha kwa kuwakumbusha wazazi kuwa utajiri wa kweli haupatikani kwa mali tu, bali kwa kuwekeza katika roho na maisha ya watoto. “Mali tutaziacha hapa duniani, lakini imani njema na malezi bora ni urithi wa milele” alisisitiza.

Dominika hii imeacha alama ya kipekee kwa waamini wa Ngulelo na Jimbo zima, ikiwahimiza kutazama upya maisha yao ya kiroho, kushikamana kama familia ya Mungu na kutembea pamoja katika njia ya Amani, Sala, na Imani thabiti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked*